Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema akiwasili mahakamani leo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa,
Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa Kibamba wakiwasili katika
Mahakama ya Rufani Arusha Leo, Jumatatu 27/02/2017 kusikiliza shauri la
Mbunge Godbless Lema.
Viongozi wengine waliofika
mahakamani leo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji,
Mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Mwesiga Baregu, Waziri Mkuu Mstaafu,
Frederick Sumaye, Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro, Katibu wa
CHADEMA Arusha, Aman Golugwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA.
ARUSHA: Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ikiongozwa na majaji
watatu, iliyokaa Arusha leo Februari 27, 2017 imetupilia mbali Rufaa
zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha kuhusu pingamizi la dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Jonathan Lema.
Wakili wa Lema, Peter Kibatala amesema kuwa tangu awali waliwaambia
serikali kuwa rufaa hizo mbili walizozifungua dhidi maamuzi ya mahakama
kuu kuwa hazikuwa na mantiki yoyote kisheria.
Hata hivyo, mahakama hiyo imetoa maelekezo kuwa jalada la kesi hiyo
lipelekwe Mahakama Kuu ili kuendelea na mchakato wa kumpatia dhamana
katika kesi inayomkabili kwani hakuna hoja ya msingi kwa rufaa
iliyokatwa na mawakili wa serikali.
Majaji wamesema wamesoma mapingamizi ya mawakili wa serikali bila
kuona tija yoyote ya kisheria kwa hiyo imetoa amri kwa Mahakama Kuu
kulishughulikia suala la Godbless Lema haraka.
Mbunge huyo aliyekamatwa Novemba 2 mwaka jana, mjini Dodoma na
kusafirishwa hadi Dar kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi, amesota
rumande kwa takribani miezi minne sasa na leo amerejeshwa tena rumande
baada ya mahakama kuamuru kesi yake iriejeshwe kwenye